• HABARI MPYA

  Monday, May 10, 2021

  ARSENAL YAICHAPA WEST BROM 3-1 NA KUISHUSHA RASMI DARAJA

   TIMU ya Arsenal jana imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yalifungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 29, Nicolas Pépé dakika ya 35 na Willian dakika ya 90, wakati la WBA limefungwa na Matheus Pereira dakika ya 67.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 52 baada ya kucheza mechi 35 katika nafasi ya tisa, wakati West Brom inabaki na pointi zake 26 za mechi 35 pia katika nafasi ya 19 na ndiyo imeshuka rasmi daraja.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA WEST BROM 3-1 NA KUISHUSHA RASMI DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top