• HABARI MPYA

  Friday, May 14, 2021

  REAL MADRID YAICHAPA GRANADA 4-1 KATIKA LA LIGA

   TIMU ya Real Madrid imeibuka na ushindi wa ugenini wa 4-1 dhidi ya Granada katika mchezo wa La Liga  Uwanja wa Nuevo Los Cármenes.
  Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Luka Modrić dakika ya 17, Rodrygo dakika ya  45, Odriozola dakika ya 75 na 76 na Karim Benzema dakika ya 76, wakati la Granada limefungwa na Jorge Molina dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi 78 baada ya kucheza mechi 36 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili Atletico Madrid baada ya wote kucheza mechi 36, wakati Granada ni ya  10 pointi zake 45 za mechi 36 sasa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAICHAPA GRANADA 4-1 KATIKA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top