• HABARI MPYA

  Monday, May 03, 2021

  INTER MILAN WATWAA UBINGWA WA SERIE A BAADA YA MIAKA 11

  TIMU ya Inter Milan imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya Italia, maarufu kama Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11 kufuatia Atalanta kulazimishwa sare ya 1-1 na Sassuolo ugenini jana.
  Sasa Inter Milan ambayo juzi iliifunga Crotone 2-0 na kufikisha pointi 82 baada ya kucheza mechi 34 ni bingwa rasmi, kwani pointi zake haziwezi kufikiwa na wapinzani, Atalanta, Juventus na AC Milan ambazo kila moja kwa sasa ina pointi 69 za mechi 34 pia. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: INTER MILAN WATWAA UBINGWA WA SERIE A BAADA YA MIAKA 11 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top