• HABARI MPYA

  Saturday, May 29, 2021

  BOCCO, MUGALU NA MORRISON WAFUNGA SIMBA SC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA NAMUNGO FC 3-1 RUANGWA

  MABINGWA watetezi, Simba SC wametoka nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Namungo ilitangulia kwa bao la Mrundi, Nzigamasabo Steve dakika ya 22, kabla ya Simba kuzinduka kipindi cha pili kwa mabao ya washambuliaji, Mkongo Chris Kope Mutshimba Mugalu dakika ya 79, John Raphael Bocco dakika ya 84 na kiungo Mghana, Bernard Morrison dakika ya 88.
  Simba SC inafikisha pointi 64 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya mahasimu wao, Yanga SC ambao pia wamecheza mechi tatu zaidi.


  Namungo FC inabaki na pointi zake 40 za mechi 29 sasa katika nafasi ya nane, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Tanzania Prisons wanaoshika nafasi ya saba, mbele ya Dodoma Jiji FC yenye pointi 39 za mechi 29 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO, MUGALU NA MORRISON WAFUNGA SIMBA SC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA NAMUNGO FC 3-1 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top