• HABARI MPYA

  Friday, May 28, 2021

  KIM POULSEN AITA 27 TAIFA STARS, WANANE WANATOKA SIMBA SC...AZAM NA YANGA ZATOA WANNE KILA TIMU

   KOCHA Mdenmark, Kim Paulsen ametaja kikosi cha wachezaji 27 cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoingia kambini Juni 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi.
  Katika kikosi hicho kuna wachezaji wanane kutoka klabu bingwa ya nchi, Simba SC, na wanne kutoka kila timu, Yanga SC na Azam FC zinazofuatia kwa ubora katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Wengine wanne wanacheza nje ya nchi, wawili hapa hapa Afrika na wawili Ulaya, wakati waliosalia wanatoka klabu mbalimbali za hapa nchini.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIM POULSEN AITA 27 TAIFA STARS, WANANE WANATOKA SIMBA SC...AZAM NA YANGA ZATOA WANNE KILA TIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top