• HABARI MPYA

  Monday, May 31, 2021

  SIMBA SC KUONDOKA KESHO KWA NDEGE KWENDA MWANZA KUMENYANA NA RUVU SHOOTING MECHI YA LIGI KUU ALHAMISI

   MABINGWA watetezi, Simba SC wanatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kesho asubuhi kwa ndege kwenda Mwanza Alhamisi watacheza mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
  Mchezo huo utafanyika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kufuatia wenyeji, Ruvu Shooting kuamua hivyo, tofauti na kawaida yao mechi zao dhidi ya Simba na Yanga kuchezea Dar es Salaam badala ya Mlandizi mkoani Pwani, ambao Uwanja wao wa Mabatini haukidhi vigezo vya mechi za mashabiki wengi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUONDOKA KESHO KWA NDEGE KWENDA MWANZA KUMENYANA NA RUVU SHOOTING MECHI YA LIGI KUU ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top