• HABARI MPYA

  Sunday, May 16, 2021

  ALLISON AFUNGA BAO LA USHINDI LIVERPOOL YAICHAPA WEST BROM 2-1

  TIMU ya Liverpool imewachapa wenyeji, West Bromwich Albion mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa The Hawthorns.
  West Bromwich walitangulia kwa bao la Hal Robson-Kanu dakika ya 15, kabla ya Mohamed Salah kuisawazishia Liverpool dakika ya 33 na kipa Alisson kufunga la ushindi dakika ya 90 na ushei akimalizia kona ya Trent Alexander-Arnold kwa kichwa.
  Kwa ushindi huo, Liverpool imefikisha pointi 63, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja ma Chelsea baada ya wote kucheza mechi 36, wakati, West Brom inabaki na pointi zake 27 za mechi 36 pia katika nafasi ya 19.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALLISON AFUNGA BAO LA USHINDI LIVERPOOL YAICHAPA WEST BROM 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top