• HABARI MPYA

  Saturday, May 22, 2021

  MSUVA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA WYDAD CASABLANCA KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva ametokea benchi zikiwa zimesalia dakika tatu na kuiwezesha klabu yake, Wydad Athletic kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya MC Alger Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca, Morocco.
  Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga SC ya nyumbani Tanzania, aliingia dakika ya 87 kuchukua nafasi ya Aymane Hassouni kabla ya Walid El Karti kuifungia bao pekee Wydad dakika ya 90 na ushei na kwa matokeo hayo wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Algiers.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA WYDAD CASABLANCA KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top