• HABARI MPYA

  Wednesday, May 05, 2021

  MAN CITY YAICHAPA PSG 2-0 NA KUTINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA

  WENYEJI, Manchester City imefanikiwa kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Etihad.
  Mabao yote ya Man City yamefungwa na mshambuliaji Mualgeria Riyad Mahrez dakika za 11 na 63 na kwa matokeo hayo, wanaingia Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kuwachapa PSG 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Paris.
  Sasa kikosi cha Pep Guardiola kitakutana na mshindi wa jumla baina ya wenyeji Chelsea na Real Madrid ya Hispania leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Madrid.
  Fainali ya Ligi ya Mabingwa itachezwa Mei 29 Uwanja wa Ataturk Olympic Jijini Istanbul nchini Uturuki.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA PSG 2-0 NA KUTINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top