• HABARI MPYA

  Tuesday, May 11, 2021

  TFF YAMFUNGIA MECHI TANO NA FAINI 500,000 BEKI WA PRISONS BENJAMIN ASUKILE KWA KUWAKASHIFU YANGA SUMBAWANGA

  BEKI wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amefungiwa mechi tano kwa kutoa maneno ya kuikashifu klabu ya Yanga Aprili 30, mwaka huu Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo imesema kwamba, pamoja na adhabu hiyo, mchezaji huyo ametozwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa hilo alilolifanya baada ya mchezo wa Hatua ya 16 Bora ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAMFUNGIA MECHI TANO NA FAINI 500,000 BEKI WA PRISONS BENJAMIN ASUKILE KWA KUWAKASHIFU YANGA SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top