• HABARI MPYA

  Saturday, May 29, 2021

  MWAKINYO AMPIGA MUANGOLA KWA KO NA KUTWAA TAJI LA WBC

  BONDIA Mtanzania Hassan Mwakinyo ametwaa taji la WBC Afrika uzito wa Super Welter baada ya kumpiga kwa Knockout (KO) raundi ya tisa Muangola Antonio Mayala usiku wa Ijumaa ukumbi wa Next Door Arena, Masaki Jijini Dar es Salaam.
  Mtanzania mwingine,  Ibrahim Mgendera 'Ibra Class' amemshinda kwa pointi Sibusiso Zingange wa Afrika Kusini katika pambano lisilo la ubingwa uzito wa Super Feather raundi nane.
  Lakini haukuwa usiku nzuri kwa Mtanzania mwingine, Shaaban Jongo maarufu kama Jongo Jongo aliyepigwa kwa KO raundi ya pili na Mnigeria, Olanrewaju Durodora katika pambano la kuwania taji a WBC Afrika uzito Cruiser.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWAKINYO AMPIGA MUANGOLA KWA KO NA KUTWAA TAJI LA WBC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top