• HABARI MPYA

  Thursday, May 27, 2021

  SIMBA SC WAZAWADIWA SH MILIONI 50 KWA KUFIKA HATUA YA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

   MDHAMINI mkuu wa Simba  kampuni ya Sportpesa leo imeikabidhi klabu hiyo zawadi ya Sh. Milioni 50 kama zawadi kwa kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Simba SC ilitinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuongoza Kundi A mbele ya mabingwa watetezi. Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na El Merreikh ya Sudan.
  Lakini safari yake katika michuano hiyo ilifikia tamati mbele ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao 4-3, ikifungwa 4-0 Johannesburg na kushinda 3-0 Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAZAWADIWA SH MILIONI 50 KWA KUFIKA HATUA YA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top