• HABARI MPYA

  Sunday, May 09, 2021

  MAN UNITED YAICHAPA ASTON VILLA 3-1 VILLA PARK

   TIMU ya Manchester United imeitandika Aston Villa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Bruno Fernandes dakika ya 52, Mason Greenwood dakika ya 56 na Edinson Cavani dakika ya 87 baada ya Aston Villa kutangulia kwa bao la Bertrand Traoré dakika ya 24.
  Kwa ushindi huo Man United inafikisha pointi 70 baada ya kucheza mechi 34, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi 10 na mahasimu wao wa Jiji, Manchester City ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.


  Aston Villa inabaki na pointi zake 48 za mechi 34 pia hivi sasa katika nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA ASTON VILLA 3-1 VILLA PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top