• HABARI MPYA

  Friday, May 14, 2021

  TFF YAZIONYA TIMU ZA DARAJA LA KWANZA KUTOPANGA MATOKEO KATIKA MECHI ZA MWISHO MWISHONI MWA WIKI HII

   SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezitahadharisha timu kutojaribu kupanga matokeo katika mechi za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza mwishoni mwa wiki.
  Ligi hiyo inatarajiwa kufikia tamati Jumamosi na Jumapili kwa mechi za Kundi A na B, huku washindi wa kwanza wakipanda moja kwa moja Ligi Kuu na watakaomaliza nafasi ya pili watakwenda kumenyana timu zitakazoshika nafasi ya 13 na 14 katika Ligi Kuu kuwania kupanda.


  Hadi sasa Mbeya Kwanza imejihakikishia kupanda kutoka Kundi A baada ya kukusanya pointi 38 katika mechi 17, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
  Katika kundi hilo, Africans Sports ya Tanga nayo imejihakikishia kucheza na moja ya timu za Ligi Kuu kuwania kupanda kutokana na pointi zake 32 za mechi 17 ambazo haziwezi kufikiwa na timu za chini yake.
  Kundi B ndio bado kuna patashika kwa sasa Geita Gold ikiwa inaongoza kwa pointi zake 34, ikifuatiwa na Pamba SC pointi 33 na KITAYOSCE pointi 30 baada ya wote kucheza mechi 15.
  Ikumbukwe idadi ya mechi Kundi B imepungua kutoka 17 hadi 15 baada ya kushushwa kwa Singida United na matokeo yake kufutwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAZIONYA TIMU ZA DARAJA LA KWANZA KUTOPANGA MATOKEO KATIKA MECHI ZA MWISHO MWISHONI MWA WIKI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top