• HABARI MPYA

  Monday, May 17, 2021

  BARCELONA YAPIGWA, REAL NA ATLETICO MADRID ZASHINDA

   WENYEJI, Barcelona wamechapwa 2-1 na Celta de Vigo katika mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Camp Nou.
  Barcelona ilitangulia kwa bao la Nahodha wake, Lionel Messi dakika ya 28, kabla ya Santi Mina kuisawazishia Celta Vigo dakika ya 38 na kufunga la ushindi dakika ya 89.
  Celta Vigo imefikisha pointi 53 katika nafasi ya nane na Barcelona inabaki na pointi zake 76 katika nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 37.


  Mechi nyingine la La Liga bao pekee la Nacho dakika ya 68 limeipa Real Madrid ushindi wa 1-0 dhidi ya Athetic Bilbao Uwanja wa San Mamés Barria.
  Nayo Atletico Madrid imeshinda 2-1 dhidi ya Osasuna Uwanja wa Wanda Metropolitano Jijini Madrid.
  Mabao ya Atletico yamefungwa na Renan Lodi dakika ya 82 na  Luis Suárez dakika ya 88, baada ya  Ante Budimir kuwatunguliza Atletico dakika ya 75.
  Atletico Madrid sasa inaongoza La Liga kwa pointi zake 83, ikifuatiwa na Real Madrid pointi 81 baada ya wote kucheza mechi 37.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA YAPIGWA, REAL NA ATLETICO MADRID ZASHINDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top