• HABARI MPYA

  Monday, May 17, 2021

  KAGERA SUGAR YAITANDIKA RUVU SHOOTING 3-1 KAITABA NA KUJIONDOA ENEO LA HATARI YA KUSHUKA DARAJA LIGI KUU

   TIMU ya Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 14, Erick Mwijage dakika ya 40 na Ally Nassor dakika ya 70, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Moses Shaaban dakika ya 34,
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar imefikisha pointi 33 baada ya kucheza mechi 30 na kusogea nafasi ya 11 kutoka ya 17, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 37 za mechi 29 sasa katika n
  afasi ya nane.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAITANDIKA RUVU SHOOTING 3-1 KAITABA NA KUJIONDOA ENEO LA HATARI YA KUSHUKA DARAJA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top