• HABARI MPYA

  Sunday, May 09, 2021

  BAYERN MUNICH WATWAA TAJI LA TISA MFULULIZO BUNDESLIGA

  WENYEJI, Bayern Munich jana wameichapa Borussia Monchengladbach 6-0 Uwanja wa Allianz Arena na kutwaa taji la tisa mfululizo la Bundesliga.
  Robert Lewandowski akifunga mabao matatu, dakika ya pili, 34 na lingine 65 kwa penalti, huku mabao mengine yakifungwa na Thomas Muller dakika ya 23, Kingsley Coman dakika ya 44 na Leroy Sane dakika ya 85.
  Kwa ushindi huo, Bayern Munich inafikisha pointi 74 baada ya kucheza mechi 32 na kuendelea kuongoza Bundesliga kwa pointi 10 zaidi ya RB Leipzig, wakati Borussia Monchengladbach inabaki na pointi zake 46 za mechi 32 katika nafasi ya saba.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH WATWAA TAJI LA TISA MFULULIZO BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top