• HABARI MPYA

  Sunday, May 09, 2021

  DRFA YAYAZUIA MASHINDANO YA KOMBE LA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN BAADA YA WAANDAAJI KUIENGUA BIN SLUM FC

   CHAMA cha SOKA Dar es Salaam (DRFA) kimeyasimamisha mashindano ya Kombe la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, maarufu kama Ramadhani Cup baada ya waandaaji kukiuka maagizo waliyopewa.
  DRFA iliagiza mechi ya Nusu Fainali kati ya Bin Slum na Afro Oil iliyovunjika irudiwe, lakini waandaaji wakakaidi agizo hilo.
  Bin Slum walituhumiwa kuwa chanzo cha vurugu zilizovunja mchezo na kuondolewa mashindanoni huku Afro Oil wakipelekwa fainali.


  Fainali ilipangwa kufanyika jana kati ya Silent Ocean na Afro Oil, lakini Jeshi la Polisi likazuia wakiwataka waandaaji wafuate agizo la DRFA.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DRFA YAYAZUIA MASHINDANO YA KOMBE LA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN BAADA YA WAANDAAJI KUIENGUA BIN SLUM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top