• HABARI MPYA

  Sunday, May 02, 2021

  LUSAJO APIGA HAT TRICK NAMUNGO FC YAICHAPA JKT TANZANIA 3-2 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF

   NAMUNGO FC imekamilisha idadi ya timu nane za Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo.
  Mabao yote ya Namungo FC leo yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Relliant Lusajo dakika ya 23, 37 na 43, wakati ya JKT Tanzania yamefungwa na Mussa Said dakika ya 71 na Najim Magulu dakika ya 88 kwa penalti.
  Namungo inaungana na Azam FC, Simba SC, Yanga SC zote za Dar es Salaam, Dodoma Jiji FC ya Dodoma, Rhino Rangers ya Tabora, Mwadui FC ya Shinyanga na Biashara United ya Mara kwenda Robo Fainali.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUSAJO APIGA HAT TRICK NAMUNGO FC YAICHAPA JKT TANZANIA 3-2 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top