• HABARI MPYA

  Wednesday, May 19, 2021

  MAN UNITED YATOA SARE YA 1-1 NA FULHAM OLD TRAFFORD

   WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya 1-1 na Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.
  United walitangulia kwa bao la Edinson Cavani dakika ya 15 akimalizia pasi ya Bruno Fernandes, kabla ya Joe Bryan kuisawazishia Fulham dakika ya 76 akimalizia pasi ya Bobby De Cordova-Reid.
  Kwa matokeo hayo, United wanafikisha pointi 71 baada ya kucheza mechi 37, ingawa wanabaki nafasi ya pili nyuma ya mabingwa tayari, Manchester City wenye pointi 83 za mechi 36, wakati Fulham inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 37 katika nafasi ya 18 wakihitaji miujiza tu kubaki Ligi Kuu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATOA SARE YA 1-1 NA FULHAM OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top