• HABARI MPYA

  Friday, May 14, 2021

  JKT TANZANIA YAWATANDIKA GWAMBINA FC 1-0 LEO MISUNGWI KATIKA MECHI YA LIGI KUU BARA

   BAO pekee la Edson Katanga dakika ya 14 leo limeipa JKT Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Gwambina FC Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.
  Kwa ushindi huo, JKT Tanzania imefikisha pointi 33 baada ya kucheza mechi 29 na kusogea nafasi ya 12, wakati Gwambina FC inabaki na pointi zake 30 za mechi 28 sasa katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 18.
  Ikumbukwe timu nne zitashuka moja kwa moja mwishoni mwa msimu na mbili zitakwenda na timu za Daraja la Kwanza kuwania kubaki Ligi Kuu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAWATANDIKA GWAMBINA FC 1-0 LEO MISUNGWI KATIKA MECHI YA LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top