• HABARI MPYA

  Sunday, May 23, 2021

  BIASHARA UNITED YAITWANGA NAMUNGO FC 2-0 MUSOMA NA KUTINGA NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

   TIMU ya Biashara United imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Namungo FC jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Mabao ya Biashara United yamefungwa na Mpapi Nasibu dakika ya tisa na Kelvin Friday kwa penalti dakika ya 39 na sasa watasubiri mshindi kati ya Mwadui FC na Yanga zinazomemyana keshokutwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga wakutane naye katika Nusu Fainali.
  Mechi nyingine za Robo Fainali zitachezwa Jumatano kati ya Rhino Rangers ya Tabora na Azam FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na Simba SC na Dodoma Jiji Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YAITWANGA NAMUNGO FC 2-0 MUSOMA NA KUTINGA NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top