• HABARI MPYA

  Thursday, May 20, 2021

  LIVERPOOL YAICHAPA BURNLEY 3-0 NA KUPANDA TOP FOUR ENGLAND

  MABINGWA wa msimu uliopita, Liverpool wameshinda mabao 3-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Turf Moor.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino dakika ya 43, Nathaniel Phillips dakika ya 52 na Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 88.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 66 baada ya kucheza mechi 37 na kupanda nafasi ya nne ikiizidi wastani wa mabao tu Leicester City, wakati  Burnley inabaki na pointi zake 39 za mechi 37 sasa katika nafasi ya 17.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA BURNLEY 3-0 NA KUPANDA TOP FOUR ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top