• HABARI MPYA

  Saturday, May 22, 2021

  BOCCO APIGA MBILI SIMBA SC YAITANDIKA KAIZER CHIEFS 3-0 LAKINI YATOLEWA LIGI YA MABINGWA

   NAHODHA John Raphael Bocco amefunga mabao mawili Simba SC ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Pamoja na ushindi huo, Simba SC imetolewa baada ya kuchapwa 4-0 katika mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
  Bocco alifunga mabao yake dakika za 24 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu na dakika ya 56 akimalizia krosi ya kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone.
  Bao la tatu la Simba limefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama baada ya juhudi zake mwenyewe kabla ya kufumua shuti kali.
  Simba SC ingeweza kuondoka na ushindi waliouhitaji kama safu yake ya ushambuliaji ingetumia vyema nafasi zote walizopata.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO APIGA MBILI SIMBA SC YAITANDIKA KAIZER CHIEFS 3-0 LAKINI YATOLEWA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top