• HABARI MPYA

  Tuesday, May 18, 2021

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 JAMHURI NA KUJIONDOA KWENYE ENEO LA HATARI YA KUSHUKA DARAJA LIGI KUU

   WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Kelvin Sabato Kongwe dakika ya 11 na George Makang'a dakika ya 61 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 30 na kusogea nafasi ya 11, wakati Mbeya City inayobaki na pointi zake 33 za mechi 30 inaangukia nafasi ya 13.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 JAMHURI NA KUJIONDOA KWENYE ENEO LA HATARI YA KUSHUKA DARAJA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top