// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIVERPOOL YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIVERPOOL YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 10, 2014

    LIVERPOOL YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA

    MWISHO wa safari. Liverpool imetupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia sare ya 1-1 nyumbani, Uwanja wa Anfield na FC Basle, hivyo kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi B.
    Fabian Frei aliifungia Basle bao la kuongoza dakika ya 25, kabla ya Lazar Markovic wa Liverpool aliyetokea benchi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 60.
    Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard aliifungia timu yake bao la kusawazisha kwa mpira wa adhabu dakika ya 80 na haikuwa ajabu alipoibuka mchezaji bora usiku huu kwa timu yake, huku mchezaji bora wa mechi akiwa Luca Zuffi wa Basle.
    Mchezo mwingine wa Kundi B, vinara Real Madrid wamiechapa mabao 4-0 RFC Ludogorets Razgrad. 
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Johnson, Lovren, Skrtel, Jose Enrique/Moreno dk45, Allen, Lucas/Coutinho dk74, Henderson na Gerrard. 

    Basle: Vaclik, Schar, Suchy, Safari, Elneny/Diaz dk83, Frei, Xhaka, Zuffi/Samuel dk88, Gashi, Gonzalez na Streller/Embolo dk74.
    Gerrard goes tumbling in the box in the second half but Basle goalkeeper Tomas Vaclik had got his hand on the ball first
    Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard alimtoka kipa wa Basle, Tomas Vaclik, lakini hakufunga kipindi cha kwanza 

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2867530/Liverpool-1-1-Basle-Reds-sent-crashing-Champions-League-despite-Steven-Gerrard-s-best-efforts.html#ixzz3LRTbDSGT 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top