// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HANS POPPE: TUMEMALIZANA NA KESSI, CALABAR NAYE ANAKUJA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HANS POPPE: TUMEMALIZANA NA KESSI, CALABAR NAYE ANAKUJA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 10, 2014

    HANS POPPE: TUMEMALIZANA NA KESSI, CALABAR NAYE ANAKUJA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imesema kwamba imefikia makubaliano na klabu ya Mtibwa Sugar juu ya mauziano ya beki wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, kikwazo cha kukamilisha dili la kumpata beki huyo kinda kimekwisha.
    “Kikwazo kilikuwa ni klabu yake, Mtibwa Sugar, lakini sasa makubaliano yamefikiwa vizuri na kinachofuata ni kumsainisha mchezaji,”amesema Hans Poppe.
    Hassan Kessy akimpitia Haruna Niyonzima wa Yanga SC 

    Mbali na hilo, Poppe amezungumzia beki wa kati, Mkenya David Owino ‘Calabar’ anayekuja kwa majaribio kutoka klabu ya ... sasa atawasili baadaye leo.
    “Huyu mchezaji tunamjua, ni mzuri na anakuja ili tumuone tu mara moja kisha tujue kama tunamsajili au vipi,”amesema Poppe. 
    Amesema Nahodha wao pia, Mganda Joseph Owino naye anatarajiwa kuja leo, baada ya awali kukosa ndege. “Kuna tatizo sasa hivi la ndege kwa safari zetu za Afrika Mashariki, lakini nadhani limetatuliwa na Owino (Joseph) atatua kesho (leo),”amesema Poppe.
    Hans Poppe kushoto akzungumza na Mkuu wa Majeshi Tanzania, Jenerali Mwamunyange
    Calabar akibinuka tik tak mbele ya John Obi Mikel wa Nigeria

    Simba SC ipo kambini visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Na kama itafanikiwa kumalizana na wachezaji wote hao wawili, Kessy na Calabar wanaweza kushiriki mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga SC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HANS POPPE: TUMEMALIZANA NA KESSI, CALABAR NAYE ANAKUJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top