• HABARI MPYA

  Tuesday, December 09, 2014

  AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 3-1 KWENYE MATAA YA CHAMAZI

   Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeifunga mabao 3-1 Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mchezo huo maalum uliondaliwa kujaribu taa za Uwanja wa Azam Complex, ulikuwa mkali na wa kusisimua baina ya timu hizo ambazo zinafukuzana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Hadi mapuzmiko tayari Azam FC walikuwa mbele kwa mabao hayo 3-1, yaliyofungwa Didier Kavumbangu dakika ya nne, Aggrey Morris dakika ya 15 na Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 45.
  Kiungo wa Azam FC, Himid Mao aliyecheza beki ya kulia leo, akimtoka mshambuliaji wa Mtibwa Mussa Hassan Mgosi 

  Himid Mao akimpongeza mfungaji wa bao la tatu la Azam, Khamis Mcha 'Vialli' kulia
  Kiungo wa Azam FC,m Salum Abubakar 'Sure Boy' akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Mtibwa, Henry Joseph  

  Kavumbangu alifunga akimalizia mpira uliookolewa na kipa kufuatia shuti dhaifu la Kipre Tchetche, wakati Morris alifunga kwa mpira wa adhabu umbali wa mita 20 na Mcha alifunga ndani ya boksi kufuatia kona ya Mudathir Yahya.
  Bao la Mtibwa lilifungwa na mkongwe Mussa Hassan Mgosi kwa penalti dakika ya 35 kufuatia beki Serge Wawa Pascal kuunawa mpira kwenye boksi.
  Kipindi cha pili, Mtibwa Sugar walijizatiti na kuonyesha upinzani zaidi kwa wenyeji wao, ingawa waliishia kukosa mabao ya wazi- sifa zimuendee kipa Mwadini Ali aliyeokoa michomo mingi ya hatari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 3-1 KWENYE MATAA YA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top