// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); COASTAL UNION KUCHEZA NA AFC ARUSHA SHEREHE ZA UHURU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE COASTAL UNION KUCHEZA NA AFC ARUSHA SHEREHE ZA UHURU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 07, 2014

    COASTAL UNION KUCHEZA NA AFC ARUSHA SHEREHE ZA UHURU

    Na Mwandishi Wetu, TANGA
    MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Coastal Union ya Tanga wanatarajiwa kusherehekea miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya AFC ya Arusha Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga Desemba 9, mwaka huu.
    Mechi hiyo ni maandalizi kwa timu hiyo kujiandaa na mechi zake za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya mapumziko ya siku 10 kutokana na Ligi kuu kusimama kwa muda ambapo itaendelea Desemba 26 mwaka huu.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari jana mjini hapa, Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ni muhimu kwa timu hiyo kujitayarisha kwa ajili ya raundi inayofuata kwenye michuano hiyo.
    Wachezaji wa Coastal Union watacheza na AFC Desemba 9 Mkwakwani

    Amesema kuwa baada ya kumalizika mechi hiyo wataangalia uwezekano wa kutafuta mechi nyengine ya majaribio kabla ya kuanza ligi hiyo ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.
    Aidha amesema kuwa timu hiyo ya AFC yenye makazi yake Mkoani Arusha inatajiwa kuwasili mkoani Tanga Desemba 8 mwaka huu kwa ajili ya mtanange huo lengo likuwa kuziandaa timu zote mbili kwa mashindano yanayowakabili.
    Amesema kuwa mechi hiyo ina umuhimu kwa timu zote mbili sisi ni kujiandaa na Michuano ya Ligi kuu Tanzania bara raundi inayofuata na wapinzania wetu  wanajiandaa na Ligi daraja la kwanza hapa nchini.
    Hata hivyo amesema kuwa mazoezi ya timu hiyo yameendelea kushika kasi kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga baada ya wachezaji wote waliokwenda mapumziko kurejea kwa asilimia kubwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION KUCHEZA NA AFC ARUSHA SHEREHE ZA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top