• HABARI MPYA

  Sunday, December 07, 2014

  BIG BULLETS WATWAA UBINGWA LIGI KUU MALAWI, GASTIN SIMKODA MFUNGAJI BORA

  Na Mwandishi Wetu, BLANTYRE
  TIMU ya Big Bullets imetawazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Malawi 2014, maarufu kama TNM Super League kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Blantyre United iliyoshuka Daraja Uwanja wa Kamuzu, Blantyre jana.
  Nahodha wa jana, Sankhani Mkandawire aliokolea kwenye mstari shuti la Abraham Kamwendo, kabla ya krosi ya winga Dalitso Siliva kuunganishwa nyavuni na Jelesi Lufeyo dakika ya 11 kuipatia Bullets bao la kwanza.
  Sports-6
  Big Bullets ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu Malawi.
  Beki wa kulia, Pilirani Zonda alifumua shuti kali baada ya kazi nzuri ya Siliva kuifungia Bullets bao la pili dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza na kipindi cha pili, Jimmy Zakazaka, alikosa mabao yasiyopungua matatu ya wazi aliunganisha krosi ya Fischer Kondowe kufunga bao la tatu dakika ya 52.
  Bullets sasa inamaliza Ligi hiyo yenye timu 15 ikiwa na pointi 62, ikiwazidi kwa pointi tisa, Moyale Barracks waliomaliza nafasi ya pili baada ya jana kufungwa 2-1 na Blue Eagles waliomaliza nafasi ya tatu.
  Kitu pekee wanachoweza kujivunia Moyale ni kutoa mfungaji bora, Gastin Simkoda aliyefunga mabao 17 wakati Karonga United, Blantyre United na Chikwawa United zote zimeshuka Daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIG BULLETS WATWAA UBINGWA LIGI KUU MALAWI, GASTIN SIMKODA MFUNGAJI BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top