• HABARI MPYA

  Wednesday, May 01, 2024

  REAL MADRID YATOA SARE 2-2 NA BAYERN MUNICH UJERUMANI


  WENYEJI, Bayern Munich wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani.
  Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na winga Mjerumani mwenye asili ya Senegal, Leroy Aziz Sané dakika ya 53 na mshambuliaji Muingereza, Harry Kane kwa penalti dakika ya 57, wakati ya Real Madrid yote yamefungwa na mshambuliaji Mbrazil, Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior dakika ya 24 na 83 kwa penalti.
  Sasa Real Madrid itatakiwa kushinda nyumbani kwenye mchezo wa marudiano au sare si za ya bao 1-1 ili kwenda Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini.
  Na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Borussia Dortmund ya Ujerumani pia na PSG ya Ufaransa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YATOA SARE 2-2 NA BAYERN MUNICH UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top