• HABARI MPYA

  Thursday, December 04, 2014

  SIMBA SC WATAMBA KUENDELEZA UBABE KWA YANGA DESEMBA 13 TAIFA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC wamesema hawana wasiwasi kabisa na pambano la Nani Mtani Jembe Jumamosi ya wiki ijayo, kwa kuwa Yanga SC ni vibonde wao wa siku zote.
  Msemaji wa Simba SC, Humphrey Nyasio amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba wana matumaini ya kuendeleza ubabe kwa Yanga.
  “Sisi hatuna wasiwasi kabisa, tunaendelea na maandalizi yetu na timu yetu leo imeingia kambini kujiandaa kuendeleza desturi yetu ya kuwanyanyasa wapinzani wetu (Yanga SC),”amesema.  
  Nani Mtani Jembe 2 inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Desemba 13, 2014 kuanzia Saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Humphrey Nyasio kushoto amesema wataendeleza ubabe kwa Yanga SC Nani Mtani Jembe 

  Pambano hili ni hitimisho la kampeni ya NMJ iliyoendeshwa kwa wiki 10 ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kwa kunywa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa klabu hizo.
  Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura ametaja viingilio vya mechi hiyo kuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP B, 20,000/= VIP C, 15,000/= kwa viti vya rangi ya chungwa kiingilio kitakuwa ni sh 15,000 huku viti vya bluu na kijani tiketi zikiuzwa kwa sh. 7,000/=.  
  Wambura amesema pambano hilo litakalosimamiwa na TFF litaanza Saa 10:00 jioni na litachezwa kwa dakika 90 tu ambapo kama muda timu hizo hazitafungana basi mikwaju ya penati itapigwa ili mshindi apatikane. 
  Taji la Nani Mtani Jembe linashikiliwa na Simba ambao waliwafunga mahasimu wao 3-1 katika mechi iliyochezwa Desemba 21, 2013. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WATAMBA KUENDELEZA UBABE KWA YANGA DESEMBA 13 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top