// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); OKWI ASIPOFIKA DAR HADI JUMAPILI, SIMBA SC ITAMCHUKULIA HATUA KALI ZA KINIDHAMU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE OKWI ASIPOFIKA DAR HADI JUMAPILI, SIMBA SC ITAMCHUKULIA HATUA KALI ZA KINIDHAMU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 05, 2014

    OKWI ASIPOFIKA DAR HADI JUMAPILI, SIMBA SC ITAMCHUKULIA HATUA KALI ZA KINIDHAMU

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI wawili wa Uganda, beki Joseph Owino na mshambuliaji Emmanuel Okwi watachukuliwa na hatua kali za kinidhamu na klabu yao, Simba SC iwapo watakuwa hawajafika Dar es Salaam hadi Jumapili.
    Wawili hao wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumapili kujiunga na klabu yao, Simba SC kwa maandalizi ya mechi ya Nani Mtani Jembe 2 wiki ijayo.
    Ofisa Habari wa Simba SC, Humphrey Nyasio ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, Owino na Okwi waliomba udhuru wa kuchelewa kidogo na klabu ikawakubalia.
    “Hawa wachezaji waliomba udhuru kidogo nasi tukawakubalia na ni matarajio yetu kwamba watarudi mwishoni mwa wiki hii kama tulivyokubaliana,”amesema.
    Emmanuel Okwi kulia asipofika Dar es Salaam hadi Jumapili Simba SC itamchukulia hatua za kinidhamu

    Alipoulizwa iwapo wachezaji hao hawatakuwa wamefika Dar es Salaam hadi Jumapili, Jumapili amesema; “Hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao,”. 
    Nani Mtani Jembe 2 inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Desemba 13, 2014 kuanzia Saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Pambano hili ni hitimisho la kampeni ya NMJ iliyoendeshwa kwa wiki 10 ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kwa kunywa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa klabu hizo.
    Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura ametaja viingilio vya mechi hiyo kuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP B, 20,000/= VIP C, 15,000/= kwa viti vya rangi ya chungwa kiingilio kitakuwa ni sh 15,000 huku viti vya bluu na kijani tiketi zikiuzwa kwa sh. 7,000/=.  
    Wambura amesema pambano hilo litakalosimamiwa na TFF litaanza Saa 10:00 jioni na litachezwa kwa dakika 90 tu ambapo kama muda timu hizo hazitafungana basi mikwaju ya penati itapigwa ili mshindi apatikane. 
    Taji la Nani Mtani Jembe linashikiliwa na Simba ambao waliwafunga mahasimu wao 3-1 katika mechi iliyochezwa Desemba 21, 2013. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI ASIPOFIKA DAR HADI JUMAPILI, SIMBA SC ITAMCHUKULIA HATUA KALI ZA KINIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top