TIMU ya Misri imefanikiwa kufuzu Hatua ya 32 Kombe la Dunia licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na Iran katika mchezo wa Kundi G Asubuhi ya leo Uwanja wa Lumen Field Jijini Seattle, Washington, Marekani.
Kiungo Mahmoud Saber Abdelmohsen Hassan Abdelmohsen anayecheza kwa mkopo ZED kutoka Pyramids, zote za kwao alianza kuifungia Misri dakika ya tano, kabla ya beki Ramin Rezaeian Semeskandi wa Foolad ya kwao pia kuisawazishia Iran dakika ya 14.
Mchezo mwingine wa mwisho wa kundi hilo, Ubelgiji imeichapa New Zealand mabao 5-1 Uwanja wa BC Place, Vancouver nchini Canada.
Mabao ya Ubelgiji yamefungwa na mshambuliaji Leandro Trossard wa mabingwa wa England, Arsenal mawili dakika ya 28 na 50, wachezaji wa Napoli ya Italia, kiungo Kevin De Bruyne dakika ya 66 na mshambuliaji Romelu Lukaku Bolingoli mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongi (DRC) dakika ya 86 na winga, au beki wa AC Milan ya Italia pia Alexis Jesse M. Saelemaekers dakika ya 90+4.
Bao pekee la New Zealand limefungwa na winga wa Motherwell ya Scotland, Elijah Henry Just anayezaliwa na baba Mjerumani na mama Mchina aliyefunga dakika ya 84.
Kwa matokeo hayo, Ubelgiji inamaliza kileleni Kundi G kwa pointi zake tano ikiizidi tu wastani wa mabao Misri n azote zimefuzu Hatua ya 32 Bora, huku Iran iliyomaliza nafasi ya tatu kwa pointi zake ikisubiri kujaribu kufuzu kama mmoja wa washindi wa tatu bora na New Zealand iliyoshika mkia kwa pointi yake moja imeaga michuano.



.png)
0 comments:
Post a Comment