• HABARI MPYA

  Friday, December 05, 2014

  MICHUANO YA WANAWAKE TAIFA CUP KUANZA DESEMBA 28

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  MICHUANO ya taifa ya soka ya wanawake ya Proin Women Taifa Cup inaanza rasmi Desemba 28 mwaka huu kwa mechi ya ufunguzi kati ya timu za mikoa ya Mara na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Kombaini za mpira wa miguu za mikoa yote ya Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo yatakayochezwa kwa raundi mbili mwanzoni, na baadaye hatua ya robo fainali hadi fainali.
  Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin Promotions Limited, kuanzia hatua ya robo fainali, mechi zote zitafanyika jijini Dar es Salaam.
  Timu ya taifa ya wanawake inatarajiwa kunufaika na mashindano hayo

  Meneja Biashara wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Peter Simon Shankunkuli aliishukuru kampuni ya Proin ambao ni watengenezaji, wazalishaji na wasambazaji wa filamu za kitanzania kwa kuwezesha mashindano hayo kufanyika kwa mara ya kwanza.
  Proin Promotions imekua ikivumbua vipaji mbalimbali vya uigizaji na sasa imeamua kujikita katika mpira wa miguu ili kuweza kuvumbua vipaji kwa wachezaji wa kike.
  Shankunkuli alisema nafasi bado zipo kwa wadhamini watakaoguswa na mashindano hayo, kwa kuwasiliana na TFF au Proin Promotions Limited kwa maelezo zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MICHUANO YA WANAWAKE TAIFA CUP KUANZA DESEMBA 28 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top