• HABARI MPYA

  Friday, December 05, 2014

  SIMBA SC YATOA SARE 0-0 NA EXPRESS

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Express ya Uganda katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Simba SC ndiyo waliouanza mchezo huo kwa kasi na ndani ya dakika 12 tayari walikosa mabao mawili ya wazi, yote kupita kwa mshambuliaji Elias Maguri. 
  Kwanza, dakika ya 10 shuti zuri la Maguri liligonga mwamba na dakika ya 12, mchezaji huyo wa zamani wa Ruvu Shooting tena akapiga kichwa kuunganisha krosi ya Ramadhani Singano ‘Messi’ mpira ukagonga mwamba.
  Express walijibu shambulizi dakika ya 15 baada ya Isaac Sserunkuma kupiga shuti kali lililokwenda nje sentimita chache. 
  Kiungo wa Simba SC, Awadh Juma akipambana kwenye eneo la hatari la Express
  Shaaban Kisiga 'Malone' wa Simba SC akiwatoka wachezaji wa Express leo Taifa

  Simba SC ilipata pigo dakika ya 27 baada ya beki wake wa kulia, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kugongana na mshambuliajin wa Express Julius Ogwang na kuumia kiasi cha kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
  Kocha wa Simba SC, Patrick Phiri kipindi cha pili alimpumzisha Elias Maguri na kumuingiza Mrundi Amisi Tambwe, ambaye dakika kwanza tu baada ya kuingia uwanjani, alikosa  bao la wazi kufuatia krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika, Nassor Masoud ‘Chollo’, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’/Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ dk30, Abdul Makame, Hassan Isihaka, Pierre Kwizera, Awadh Juma, Abdallah Seseme/Omar Mboob dk76, Elias Maguri/Amisi Tambwe dk46, Shaaban Kisiga ‘Malone’/Ibrahim Hajibu dk87 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Twaha Ibrahim ‘Messi’ dk87.
  Express; Mutumba Ivan, Bakari Shafiq, Hassan Wasswa/Emma Kakyowa dk64, Henri Katongile, Bob Kasozi, Ivan Sserunkuma, Thadeo Lwanga, Willy Kavuma, Julius Ogwang, Simon Sserunkuma na Isaac Sserunkuma/John Semazi dk72.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATOA SARE 0-0 NA EXPRESS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top