// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); EMERSON WA YANGA KAMA NI GALASA AU KIFAA TUTAJUA KESHO MECHI NA EXPRESS TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE EMERSON WA YANGA KAMA NI GALASA AU KIFAA TUTAJUA KESHO MECHI NA EXPRESS TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 05, 2014

    EMERSON WA YANGA KAMA NI GALASA AU KIFAA TUTAJUA KESHO MECHI NA EXPRESS TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mpya Mbrazil wa Yanga SC, Emerson de Oliviera Roque (pichani kulia) kesho anatarajiwa kuichezea klabu yake hiyo mpya kwa mara ya kwanza itakapomenyana na Express ‘Tai Mwekundu’ kutoka Kampala, Uganda.
    Mchezo huo wa kirafiki, unaotarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni Uwanja Taifa, Dar es Salaam, unatarajiwa kuwapa fursa mashabiki wa timu hiyo kujionea kuhusu kiungo huyo mkabaji.
    Emersom amesajiliwa kuchukua nafasi ya Mbrazil mwingine, mshambuliaji Genilson Santana Santos ‘Jaja’, aliyejitoa kwenye timu hiyo baada ya miezi mitano kwa matatizo ya kifamilia. 
    Kwa Yanga SC, inayofundishwa na Mbrazil pia Marcio Maximo, zaidi mchezo huo utakuwa sehemu ya kukipima kikosi chake kabla ya mchezo wa Nani Mtani Jembe 2, dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC.
    Nani Mtani Jembe 2 inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Desemba 13, 2014 kuanzia Saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Pambano hili ni hitimisho la kampeni ya NMJ iliyoendeshwa kwa wiki 10 ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kwa kunywa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa klabu hizo.
    Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura ametaja viingilio vya mechi hiyo kuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP B, 20,000/= VIP C, 15,000/= kwa viti vya rangi ya chungwa kiingilio kitakuwa ni sh 15,000 huku viti vya bluu na kijani tiketi zikiuzwa kwa sh. 7,000/=.  
    Wambura amesema pambano hilo litakalosimamiwa na TFF litaanza Saa 10:00 jioni na litachezwa kwa dakika 90 tu ambapo kama muda timu hizo hazitafungana basi mikwaju ya penati itapigwa ili mshindi apatikane. 
    Taji la Nani Mtani Jembe linashikiliwa na Simba ambao waliwafunga mahasimu wao 3-1 katika mechi iliyochezwa Desemba 21, 2013. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EMERSON WA YANGA KAMA NI GALASA AU KIFAA TUTAJUA KESHO MECHI NA EXPRESS TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top