• HABARI MPYA

  Friday, December 05, 2014

  RAIS KENYATTA AWAALIKA IKULU SOFAPAKA BAADA YA KUTWA NGAO GOtv

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  RAIS wa taifa la Kenya Uhuru Muigai Kenyatta jana Alhamisi aliwaandalia karamu fupi mabingwa wa Ngao ya GOtv Sofapaka kwenye ikulu.
  Baada ya kuwapongeza kwa kuwai taji hilo lililowapa tiketi ya kuakilisha Kenya kwenye michuano ya mashirikisho barani Afrika mwaka ujao, rais aliwazawidi shilingi milioni moja pesa za Kenya (takribani milioni kumi na tisa pesa za Tanzania).
  “Wawekezaji wa spoti wamo humu nchini kukuza vipaji hivo tusaidiane ili kufanikisha hilo, tusiiingilie mipango yao,” alisema Kenyatta wakati wa hafla hiyo.
  Rais Kenyatta kulia akisalimiana na wachezaji wa Sofapaka mjini Nairobi jana


  Sofapaka waliwapiku Posta Rangers 2 – 1 kwenye fainali iliyosakatwa Novemba 15 mjini Nakuru kupitia kwa magoli yao Enock Agwanda na Clifton Miheso huku aliyekuwa beki wa Simba SC Paschal Ochieng’ akifunga la Kutoa machozi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS KENYATTA AWAALIKA IKULU SOFAPAKA BAADA YA KUTWA NGAO GOtv Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top