• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  BALOTELLI AKUTWA NA HATIA, APEWA HADI DESEMBA 15 KUJIBU MASHITAKA

  MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekuwa na hatia na Chama cha Soka England baada ya kuposti picha inayodaiwa ya udhalilishaji kwenye mtandao wa kijamii.
  FA imesema Balotelii amekutwa na hatia kwa kuvunja sheria  E3 (1) na Mtaliano amepewa hadi Saa 12:00 jioni ya Desemba 15 kusema namna gani atajibu kesi yake.
  Balotelli anakabiliwa na adhabu kama ya beki wa QPR, Rio Ferdinand ambaye kwa kuvunja sheria E3 Oktoba mwaka huu, Nahodha huyo wa zamani wa Manchester United alifungiwa mechi tatu na kupigwa faibi ya Pauni 25,000 kwa kuweka picha ya udhalilishaji kwenye akaunti yake ya Tweeter. Ferdinand pia aliwahi kutozwa faini ya Pauni 45,000 mwaka 2012 kwa kumdhalilisha beki wa wakati huo wa Chelsea, Ashley Cole akimuita 'choc ice' kwenye Twitter.
  Liverpool striker Mario Balotelli has been charged by the FA for a controversial image posted to Instagram
  Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli amekutwa na hatia na FA kwa picha ya utata aliyoposti kwenye akaunti yake ya Instagram 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALOTELLI AKUTWA NA HATIA, APEWA HADI DESEMBA 15 KUJIBU MASHITAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top