// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ARSENAL YAFUMULIWA 3-2 NA STOKE , CROUCH AFUNGA BAO LA REKODI ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ARSENAL YAFUMULIWA 3-2 NA STOKE , CROUCH AFUNGA BAO LA REKODI ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 06, 2014

    ARSENAL YAFUMULIWA 3-2 NA STOKE , CROUCH AFUNGA BAO LA REKODI ENGLAND

    ARSENAL imechapwa mabao 3-2 ugenini na Stoke City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
    Mabao ya Peter Crouch dakika ya kwanza, Bojan Krkic dakika ya 35 na Jonathan Walters dakika ya 45, yaliifanya Stoke iongoze 3-0 hadi mapumziko, kabla ya Gunners kuanza kupambana kurudisha.
    Crouch ameweka rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi katika Ligi Kuu ya England, kwani ilimchukua sekunde 19 tu kumuinamisha Arsene Wenger. 
    Arsenal ilipata mabao yake kupitia kwa Santi Cazorla kwa penalti dakika ya 68 na Aaron Ramsey dakika ya 70.
    Calum Chambers alionyeshwa kadi nyekundu ya kwanza nyekundu tangu aanze soka baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 78.
    Kikosi cha Stoke City kilikuwa; Begovic, Bardsley, Shawcross, Muniesa/Whelan dk63, Pieters, Nzonzi, Cameron, Diouf/Adam dk69, Bojan/Huth dk86, Walters na Crouch.
    Arsenal; Martinez, Bellerin/Welbeck dk46, Chambers, Mertesacker, Gibbs/Campbell dk90, Flamini, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Sanchez, Cazorla, Giroud/Podolski dk63.
    Peter Crouch is the toast of Stoke after opening the scoring for the Potters against Arsenal after one minute
    Peter Crouch akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Stoke bao la kwanza dhidi ya Arsenal sekunde ya 19
    Olivier Giroud scratches his head as he waits to restart with Santi Cazorla after the third goal on the stroke of half-time
    Olivier Giroud akijikuna kichwa huku Santi Cazorla akimsubiri aanzishe mpira baada ya kufungwa bao la tatu kabla ya mapumziko

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2863562/Stoke-3-2-Arsenal-Peter-Crouch-leads-Potters-half-spree-Gunners-fight-stalls-Calum-Chambers-sent-off.html#ixzz3L8s5xqRo 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAFUMULIWA 3-2 NA STOKE , CROUCH AFUNGA BAO LA REKODI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top