// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SCHOLES BADO WAMO, ATUPIA MBILI MECHI YA MAGWIJI NYOTA DUNIANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SCHOLES BADO WAMO, ATUPIA MBILI MECHI YA MAGWIJI NYOTA DUNIANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 06, 2014

    SCHOLES BADO WAMO, ATUPIA MBILI MECHI YA MAGWIJI NYOTA DUNIANI

    KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes jana ameiongoza timu ya marafiki wa Cannavaro kuifunga mabao 8-5 timu ya marafiki wa Figo katika mechi ya magwiji iliyochezwa nchini Thailand wiki hii.
    Scholes, ambaye alistaafu mwaka 2013, alitamba katika mechi hiyo akimtungua kipa wa zamani wa Arsenal, Jens Lehmann.
    Patrick Berger alianza kuwafungia akina Cannavaro kabla ya Davor Suker kusawazisha na Clarence Seedorf kufunga la pili, Cafu la tatu.
    Paul Scholes aliwarudisha mchezoni akina Cannavaro kwa kuwafungia bao la pili na baadaye akasawazisha na kuwa 3-3. Dwight Yorke akawainua akija Figo kwa kufunga bao la nne kabla ya Andriy Shevchenko kusawazisha.
    Robbie Fowler akawafungia akina Figo bao la tano kabla ya Therdsak Chaiman kusawazisha na Michel Salgado kuwafungia la sita akija Cannavaro, Kluivert la saba na Therdsak Chaiman la nane.Scholes rifles home his second goal as his team, captained by Fabio Cannavaro, won the game 8-5
    Players from both teams pose together after the game, the first of four charity matches in Asia

    Kikosi cha akina Figo kilikuwa; Jens Lehmann, Cafu, Ronald De Boer, Gianluca Zambrotta, Alessandro Nesta, Javier Zanetti, Clarence Seedorf, Luis Figo (Nahodha), Youri Djorkaeff, Vladimir Smicer, Deco, Karl-Heinz Reidle, Davor Suker, Andriy Shevchenko na Robbie Fowler.
    Timu ya Cannavaro; Jerzy Dudek, Michel Salgado, Fabio Cannavaro (Nahodha), Marco Materazzi, Juliano Belletti
    Paul Scholes, Christian Karambeu, Steve McManaman
    Hidetoshi Nakata, Patrick Berger, Rai Oliveira, Dwight Yorke
    Jari Litmanen, Patrick Kluivert na Michael Owen. 

    PICHA ZAIDI NA VIDEO NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2863328/Paul-Scholes-scores-brilliant-chip-legends-match-Real-Madrid-legend-Michel-Salgado-steals-bicycle-kick.html#ixzz3L8OOUdyB 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SCHOLES BADO WAMO, ATUPIA MBILI MECHI YA MAGWIJI NYOTA DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top