• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  SSERUNKUMA KUTAMBULISHWA KESHO SIMBA SC IKIMENYANA NA MTIBWA SUGAR CHAMAZI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC, Dan Sserunkuma atatua Dar es Salaam kesho mchana na moja kwa moja kwenda kutambulishwa mbele ya mashabiki wa Simba SC.
  Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia ya Kenya, atakwenda kuwapungia mkono mashabiki wa Simba SC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam ambako Wekundu hao wa Msimbazi watakuwa na mchezo wa kirafiki na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  Sserunkuma atatua na Waganda wenzake wanaofanya kazi Simba SC, beki Joseph Owino ambaye pia ni Nahodha wa klabu na mshambuliaji Emmanuel Okwi.
  Dan Sserunkuma atatua kesho Dar es Salaam

  Watatu hao wote hawatacheza kesho dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wataanza mazoezi Jumatatu na wenzao kujiandaa na mechi ya Nani Mtani Jembe, Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Simba SC kesho itacheza mechi ya pili ya kujipima nguvu ndani ya siku tatu, baada ya jana kutoa sare ya bila kufungana na Express ya Uganda Uwanja wa Taifa, ambayo leo imefungwa 1-0 na Yanga SC, bao la Mganda Hamisi Kiiza dakika ya 90 na ushei.
  Kocha Patrick Phiri raia wa Zambia anatumia mechi hizo kama sehemu ya maandalizi yake ya mchezo wa Nani Mtani Jembe 2, Desemba 13, mwaka huu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SSERUNKUMA KUTAMBULISHWA KESHO SIMBA SC IKIMENYANA NA MTIBWA SUGAR CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top