• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 05, 2021

  YANGA SC WALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA JAMHURI FC YA PEMBA KATIKA KOMBE LA MAPINDUZI LEO ZANZIBAR


  VIGOGO, Yanga SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Pemba katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Huo ulikuwa mchezo wa pili tu wa mashindano ya msimu huu, baada ya leo jioni mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar kushinda 1-0 dhidi ya Chipukizi, bao pekee la Ibrahim Ahmada 'Hilika' dakika ya 58 Uwanja wa Amaan.
  Kwa ujumla, Kundi A kuna Yanga SC, Namungo FC ya Lindi na Jamhuri FC ya Pemba, Kundi B kuna Simba SC, Mtibwa Sugar na Chipukizi FC na Kundi C kuna Azam FC, Malindi FC na Mlandege FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA JAMHURI FC YA PEMBA KATIKA KOMBE LA MAPINDUZI LEO ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top