• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 07, 2021

  SIMON MSUVA AIPELEKA WYDAD CASABLANCA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amecheza kwa dakika 86 kabla ya kumpisha Zouheir El-Moutaraji, Wydad Athletic Club, maarufu Wydad Casablanca ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Stade Malien de Bamako katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca.
  Mabao ya Wydad yalifungwa na A. El Kaabi dakkika ya 43, Muaid Ellafi dakika ya 46 na 64 na kwa ushindi huo Wydad inaingia hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya kuchapwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Mali.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMON MSUVA AIPELEKA WYDAD CASABLANCA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top