• HABARI MPYA

  Friday, January 29, 2021

  AL HILAL YAZINDUKA NA KUICHAPA TP MAZEMBE 2-1 DAR MICHUANO YA SIMBA SUPER CUP

  TIMU ya Al Hilal ya Sudan imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa michuano maalum ya Simba Super Cup leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Al Hilal iliyochapwa 4-1 na wenyeji, Simba SC katika mchezo wa kwanza juzi, yamefungwa na Bonganga Vinny dakika ya 30 na Mohamed Musa dakika ya 90 baada ya TP Mazembe kutangulia kwa bao la Moustapha Kouyate dakika ya 12.
  Michuano hiyo itakamilishwa Jumapili kwa mchezo kati ya wenyeji, Simba SC na TP Mazembe.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL HILAL YAZINDUKA NA KUICHAPA TP MAZEMBE 2-1 DAR MICHUANO YA SIMBA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top