• HABARI MPYA

    Thursday, January 07, 2021

    SIMBA SC WAACHANA NA VANDENBROECK SIKU MOJA BAADA YA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Simba jana imetangaza kuachana na kocha wake, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck na kwa kipindi hiki timu itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Suleiman Matola.
    Taarifa ya Simba SC imesema kwamba Bodi ya Wakurugenzi wa klabu imefikia hatua ya kuachana na Vandenbroeck baada ya maridhiano ya pande zote mbili.
    Vanderbroeck, mwenye umri wa miaka 41 anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza timu kwenye mechi 69 za mashindano yote, zikiwemo za kirafiki na kushinda 53, sare 10 na kufungwa sita tangu awasili Desemba 15 mwaka juzi, 2019.

    Katika kipindi hicho ameiwezesha timu kutwaa mataji matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka nchini (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Na ameondoka siku moja baada ya kuiwezesha Simba kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya FC Platinums ya Zimbabwe Jumatano Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
    Simba SC imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza mjini Harare – hiyo ikiwa mara ya tatu kwa Wekundu hao wa Msimbazi kutinga hatua hiyo baada ya mwaka 2003 walipoitoa Zamalek ya Misri waliokuwa mabingwa watetezi na 2018 walipoitoa Nkana FC ya Zambia.
    REKODI YA SVEN LUDWIG VANDENBROECK SIMBA SC
    1. Simba SC 6-0 AFC Arusha (Kombe la TFF Uhuru)
    2. Simba SC 4-0 Lipuli FC (Ligi Kuu Uhuru)
    3. Simba SC 2-0 KMC (Ligi Kuu Uhuru)
    4. Simba SC 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Taifa)
    5. Simba SC 2-2 Yanga SC (Ligi Kuu Taifa)
    6. Simba SC 3-1 Chipukizi FC (Kombe la Mapinduzi Gombani)
    7. Simba SC 0-0 (Penalti 3-2) Azam FC (Kombe la Mapinduzi Amaan)
    8. Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar  (Fainali Kombe la Mapinduzi Amaan)
    9. Simba SC 2-1 Mbao FC  (Ligi Kuu Kirumba)
    10. Simba SC 4-1 Alliance FC  (Ligi Kuu Kirumba)
    11. Simba SC 2-1 Mwadui FC  (Kombe la TFF Taifa)
    12. Simba SC 3-2 Mwadui FC  (Ligi Kuu Taifa)
    13. Simba SC 2-0 Coastal Union  (Ligi Kuu Taifa)
    14. Simba SC 2-1 Polisi Tanzania  (Ligi Kuu Taifa)
    15. Simba SC 0-1 JKT Tanzania  (Ligi Kuu Uhuru)
    16. Simba SC 3-0 JKT Tanzania  (Ligi Kuu Jamhuri)
    17. Simba SC 1-0 Lipuli FC  (Ligi Kuu Samora)
    18. Simba SC 1-0 Kagera Sugar  (Ligi Kuu Taifa)
    19. Simba SC 3-1 Biashara Unted  (Ligi Kuu Taifa)
    20. Simba SC 1-1 (Penalti 3-2) Stand United  (Kombe la TFF Shinyanga)
    21. Simba SC 2-0 KMC  (Ligi Kuu Taifa)
    22. Simba SC 3-2 Azam FC  (Ligi Kuu Taifa)
    23. Simba SC 0-1 Yanga SC  (Ligi Kuu Taifa)
    24. Simba SC 8-0 Singida United  (Ligi Kuu Taifa)
    25. Simba SC 4-2 Transit Camp (Kirafiki Mo Simba Arena)
    26. Simba SC 3-1 KMC (Kirafiki Mo Simba Arena)
    27. Simba SC 1-1 Ruvu Shooting  (Ligi Kuu Taifa)
    28. Simba SC 3-0 Mwadui FC  (Ligi Kuu Taifa)
    29. Simba SC 5-0 African Lyon (Kirafiki Taifa)
    30. Simba SC 2-0 Mbeya City (Ligi Kuu Sokoine)
    31. Simba SC 0-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Sokoine)
    32. Simba SC 2-0 Azam FC (Kombe la TFF Taifa)
    33. Simba SC 0-0 Ndanda SC (Ligi Kuu Nangwanda Sijaona)
    34. Simba SC 0-0 Namungo FC (Ligi Kuu Majaliwa, Ruangwa)
    35. Simba SC 4-1 Yanga SC (Kombe la TFF Taifa)
    36. Simba SC 2-3 Mbao FC (Ligi Kuu Taifa)
    37. Simba SC 5-1 Alliance FC (Ligi Kuu Taifa)
    38. Simba SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Taifa)
    39. Simba SC 2-1 Polisi Tanzania (Ligi Kuu Ushirika, Moshi)
    40. Simba SC 2-1 Namungo FC (Kombe la TFF Sumbawanga)
    41. Simba SC 6-0 Vital’O (Kirafiki Simba Day)
    42. Simba SC 3-1 KMC (Kirafiki Uhuru asubuhi)
    43. Simba SC 5-2 Transit Camp (Kirafiki Uhuru asubuhi)
    44. Simba SC 2-0 Namungo FC (Ngao ya Jamii Arusha)
    45. Simba SC 6-0 AFC Arusha (Kirafiki Arusha)
    46. Simba SC 2-1 Ihefu SC (Ligi Kuu Sokoine)
    47. Simba SC 2-1 Ihefu SC (Ligi Kuu Sokoine)
    48. Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Jamhuri)
    49. Simba SC 4-0 Biashara United (Ligi Kuu Mkapa)
    50. Simba SC 2-0 African Lyon (Kirafiki Chamazi)
    51. Simba SC 3-0 Gwambina FC (Ligi Kuu Mkapa)
    52. Simba SC 4-0 JKT Tanzania (Ligi Kuu Jamhuri)
    53. Simba SC 3-1 Mlandege SC (Kirafiki Chamazi)
    54. Simba SC 0-1 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Sumbawanga)
    55. Simba SC 0-1 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Uhuru)
    56. Simba SC 5-0 Mwadui FC (Ligi Kuu Uhuru)
    57. Simba SC 2-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Uhuru)
    58. Simba SC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu Mkapa)
    59. Simba SC 0-0 Africans Sports (Kirafiki Chamazi)
    60. Simba SC 7-0 Coastal Union (Ligi Kuu Sheikh Amri Abeid)
    61. Simba SC 1-0 Plateau United (Ligi ya Mabingwa Jos, Nigeria)
    62. Simba SC 0-0 Plateau United (Ligi ya Mabingwa Mkapa)
    63. Simba SC 2-0 Polisi Tanzania (Ligi Kuu Mkapa)
    64. Simba SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu, Sokoine)
    65. Simba SC 1-0 KMC (Ligi Kuu, Mkapa)
    66. Simba SC 0-1 FC Platinums (Ligi ya Mabingwa, Harare)
    67. Simba SC 5-0 Maji Maji FC (Kombe la TFF, Mkapa)
    68. Simba SC 4-0 Ihefu SC (Ligi Kuu, Mkapa)
    69. Simba SC 4-0 Platinums FC (Ligi ya Mabingwa, Mkapa) 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAACHANA NA VANDENBROECK SIKU MOJA BAADA YA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top