• HABARI MPYA

  Saturday, January 09, 2021

  ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA SC MBELGIJI SVEN LUDWIG VANDENBROECK AJIUNGA NA FAR RABAT YA MOROCCO

  ALIYEKUWA kocha wa Simba SC, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na ASFAR Rabat ya Morocco.
  Vandenbroeck amejiunga na timu hiyo Rabat siku moja mbili baada ya kuondoka Simba SC akitoka kuiwezesha kufuzu Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Jumatano ikiitoa FC Platinum kwa jumla ya mabao 4-1.
  Katika kipindi cha mwaka mmoja na ushei wa kuwa na Simba, Vandenbroeck ameiwezesha timu hiyo kushinda mataji matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC),


  Alijiunga na Simba SC Desemba 15 mwaka 2019 akichukua nafasi ya Mbelgiji mwenzake, Patrick Aussems.
  Vanderbroeck, mwenye umri wa miaka 41 anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza timu kwenye mechi 69 za mashindano yote, zikiwemo za kirafiki na kushinda 53, sare 10 na kufungwa sita tangu awasili Desemba 15 mwaka juzi, 2019.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA SC MBELGIJI SVEN LUDWIG VANDENBROECK AJIUNGA NA FAR RABAT YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top