• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 10, 2021

  ZIDANE ALALAMIKA MECHI YA REAL NA OSASUNA KUTOAHIRISHWA


  KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kwamba mechi yao ya La Liga dhidi ya wenyeji Osasuna iliyomalizika kwa sare ya bila mabao jana Uwanja wa El Sadar ilipaswa kuahirishwa baada ya Los Blancos kuchelewa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
  Real Madrid sasa wanazidiwa pointi moja tu na Atletico Madrid (38-37) ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi baada ya mechi yao ya jana pia dhidi ya Athletic Bilbao kuahirishwa kutokana na matatizo ya usafiri pia.
  Ndege za Madrid zilichelewa kwa saa kadhaa kutokana na Uwanja wa Ndege wa Jiji hilo kufungwa kwa muda na utaendelea kufungwa hadi angalau leo
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZIDANE ALALAMIKA MECHI YA REAL NA OSASUNA KUTOAHIRISHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top