• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 07, 2021

  THOMAS ULIMWENGU AIPELEKA TP MAZEMBE HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu jana amefunga bao la kwanza dakika ya 14, TP Mazembe ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Bouenguidi FC ya Liberia katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi.
  Bao la pili la Mazembe lilifungwa Mzambia Tandi Mwape dakika ya 45, wakati bao pekee la Bouenguidi FC lilifungwa na Djoe Dayan Boussougou dakika ya 79 na sasa wanakwenda hatua ya makundi ya michuano hiyo. Mechi ya kwanza pia Ulimwengu alifunga mabao mawili Jijini Libreville, Mazembe wakishinda 2-1 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: THOMAS ULIMWENGU AIPELEKA TP MAZEMBE HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top