• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 11, 2021

  YANGA SC WANG'ARA ZANZIBAR, WAITOA AZAM FC KWA MATUTA NA KUTANGULIA FAINALI YA KOMBE LA MAPINDUZI

  YANGA SC imefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  
  Fainali itachezwa Jumatano na Yanga SC itakutana na mshindi wa mchezo unaofuatia Saa 2:15 usiku baina ya Simba SC na Namungo FC hapo hapo Uwanja wa Amaan.  
  Winga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tuisila Kisinda alianza kuifungia Yanga SC dakika ya 52, kabla ya mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa kuisawazishia Azam FC dakika ya 67.


  Na katika mikwaju ya penalti kipa Benedict Haule aliokoa penalti moja tu, ya kwnaza iliyopigwa na mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong lakini za Kisinda, Mkongo mwingine kiungo Tonombe Mukoko, mabeki Paul Godfrey 'Boxer', Abdallah Shaibu 'Ninja' na kiungo mzawa, Zawadi Mauya zikampita kwa staili tofuti.
  Kipa Mkenya wa Yanga SC aliokoa penalti mbili, ya kwanza iliyopigwa na kiungo mzawa Awesu Awesu na ya mwisho iliyopigwa na beki Mghana, Daniel Amoah - lakininza beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa, viungo Mnyarwanda Ally Niyonzima, mzawa Mudathir Yahya na beki Mganda, Nicholas Wadada zikampita. 
  Mara ya mwisho Yanga SC kufika Fainali Kombe la Mapinduzi ilikuwa ni mwaka 2011 wakafungwa na mahasimu wao, Simba SC 2-0 mabao ya Shijja Mkina na Mussa Mgosi.
  Kwa ujumla Yanga SC imecheza fainali ya Kombe la Mapinduzi mara mbili tu, nyingine mwaka 2007 walipochukua ubingwa kwa kuifunga Mtibwa Sugar.
  ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
  Mwaka            Bingwa Mshindi wa Pili
  2007 Yanga SC Mtibwa Sugar 
  2008 Simba SC Mtibwa Sugar
  2009 Miembeni        KMKM
  2010 Mtibwa Sugar         Ocean View
  2011 Simba SC  Yanga SC
  2012 Azam FC          Simba SC
  2013 Azam FC    Tusker FC
  2014 KCCA        Simba SC
  2015 Simba SC Mtibwa Sugar
  2016 URA Mtibwa Sugar
  2017 Azam FC Simba SC
  2018 Azam FC URA FC
  2019 Azam FC Simba SC 2-1 
  2020 Mtibwa Sugar         Simba SC 1-0
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WANG'ARA ZANZIBAR, WAITOA AZAM FC KWA MATUTA NA KUTANGULIA FAINALI YA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top